ndefu
seebait
MICHEZO

Kuhusu Simba kutaka kumsajiri huyu Beki Mghana, kadai anamiaka 23

tangazo 2

Haha Simba bhana, nimeona hii picha nimecheeka sana. Huyu anaitwa Jean Ourage Vital. Huyu jamaa bhana kijiweni kwetu habari yake ilifika tokea mwezi februari mwaka huu ambapo nakumbuka alikuja kwa majaribio.
:
Anaandika @privaldinho
:
✍️Nilipenyezewa na mwana kijiwe mmoja wa klabu ya Simba. Nadhani nyote mnakumbuka enzi zile Simba ikihangaika na wachezaji kwa ajili ya CAF mixa kumleta Zana.
:
✍️Vital alitaka klabu ya Simba itoe dau la $150,000 nadhani ni kwenye milioni 34 hivi na laki tano. Lakini wakashindwana kwenye mambo binafsi kama ile ishu ya Ajibu na Mazembe.
:
✍️ Wala sio mara yake ya kwanza kufanya majaribio sehemu mbalimbali, Jamaa huyu mwenye miaka 23 kama mnavyomuona pichani, alikwenda Supersport ya Afrika Kusini akafeli, akaja TP Mazembe nae kama Ajibu wakashindwana, hivo hivo.
:
✍️ Jamaa wakati anakuja Simba alikuwa ametokea Karela United ya Ghana ambayo ilishushwa daraja mwaka jana.
:
✍️ Kwenye kijiwe changu nina mshkaji wangu yupo Ghana anaitwa Enoch Ntiamoah nikamwendea hewani, nikamuuliza unamjua Vital, akaniambia ndio, ni jamaa mmoja mwenye nyama nyama anachafua sana dimba la kati, Asante Kotoko walikuwa wanamfukuzia lakini dili lake likaingia mizengwe.
:
✍️ Akaniuliza na mimi si yupo Tanzania, nikamwambia nimemuona ndio maana nimeuliza. Baada ya wiki akaniambia kuwa jamaa kwa sasa yupo Buildcom ya Zambia. Baada ya kushindwana na Simba akaelekea zake zambia.
:
✍️Sasa hizi picha ni za zamani, unless awe amepita kijiweni kwangu kimya kimya au iwe Mo amemrudia tena jambo ambalo nadhani sasa dau lake linakwenda juu zaidi. Ila jamaa ana miaka 23 wazee. Miaka 23 tu.
:
✍️ Kama amesaini Simba upya fresh, ila jamaa ana miaka 23 tu. Halafu nimekumbuka huko Buildcom alikwenda kwa mkopo wa miezi minne, nadhani mkopo umiesha so kama amerudi Msimbazi baridi ila jamaa ana miaka 23 tu. Nimesisitiza umri kwa maana leo akija Simba akicheza miaka 3 atakua na 26 hapo Simba inaweza kumuuza bilioni 1 nawaza tu. Kwa huo umri wake. Umri wake ni potential sana. Miaka 23 sio mchezo ati.

KITU
Tags
taboola

Related Articles

Close