ndefu
seebait
MICHEZO

Kauli ya wakala wa Kagere baada ya Zamalek kumtaka kwa bilioni 1.2

tangazo 2

– PATRICK GAKUMBA AMBAYE NI WAKALA WA MEDDIE KAGERE, KAFUNGUKA KUHUSU NYOTA HUYO KUTUA ZAMALEK… Hii leo kumeibuka taarifa kwamba @simbasctanzania imepata Tshs 1.2b kumuuza Mrwanda wao kwenda kwa miamba hao wa Misri..
:
— “Ningependa kuwatangazia Watanzania, na watu wa East Africa na Mashabiki wa mpira wa miguu na hususa ni Mashabiki wa Simba SC Wekundu wa Msimbazi, kwamba habari mlizoona kuwa Meddie Kagere “MK14” Amenunuliwa na Zamalek “SIO KWELI”… Mimi Kama agent wake Super Manager nazungumza, Walio andika hizo habari nadhani ni Wapinzani waliotaka tu kuchemsha tu vichwa vya Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi lakini sio Kweli”
.
— Hapa nilipo nipo na Kagere tupo tunaelekea Gisenyi kidogo (Rwanda) tupo kwenye gari naendesha nipo na MK14 tunaenda kula Maisha kidogo… Kwahiyo hizo habari tunaziona Kama mnavyoziona… Simba ndio timu yenye uwezo wa kuzungumza kuhusu timu inayomtaka MK14 sio watu wa Nje, kwa Sababu bado wapo kwenye Mkataba.
.
— “Mimi ni professional Agent na Mchezaji wangu ni professional Player hatuwezi kufanya mambo ya kijinga au mambo ambayo hayaeleweki ya kuwa na tamaa ya Kusaini huku na kule… Woote walio andika hivi ni unprofessional journalists, uwezi kupost vitu ambavyo havina uhakika wala uthibitisho…

KITU
Tags
taboola

Related Articles

Close